Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, May 28, 2014

..MREMBO ACHANWA NA VIWEMBE KWA WIVU..

INASIKITISHA sana! Stela Mbinga ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Tegeta - Kontena jijini Dar amepata balaa kubwa baada ya kuchanwachanwa uso wake kwa viwembe na jirani yake aliyefahamika kwa jina la Zakia Mohamed.

Stella Mbinga akiwa na majeraha ya viwembe.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, Zakia na Stella kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi maisha ya uhasama na kuringishiana hali iliyojenga chuki miongoni mwao.“Hawa huwa wanashindana kimaisha. Huyu akifanya hivi, mwingine anafanya vile. Cha kushangaza huwa wanatishiana hadi mambo ya vyakula, kwamba nani anakula vizuri zaidi ya mwenzake.
“Sasa juzi Stella alikuwa amekaa kibarazani wanazungumza na shoga yake, Zakia alipita akawakuta wanacheka, hata alipokuwa chumbani wakaendelea na vicheko vyao, akahisi wanamsema na kumcheka yeye, alipotoka akamvaa Stella, kumbe alikuwa na kiwembe, akaanza kumchana bila huruma,” alisema mmoja wa majirani wa wanawake hao.
Wasamaria wema walimpeleka Stella Kituo cha Polisi Tegeta ambapo ilifunguliwa kesi nambari TGT/RB/1969/2014 - Kujeruhi kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala ambako alishonwa nyuzi 19 usoni na nane kifuani.
Stella akiuguza majeraha.
Akizungumza kwa tabu nyumbani kwake, Stella alisema: “Amenionea tu, hapa sijisikii vizuri. Nahisi kizunguzungu na giza kila ninaposimama, pia siwezi kula vizuri chakula kwani kila ninapotafuna, kichwa kinaniuma sana.”

No comments: