Unaikumbuka nyimbo ya Ice Cream iliyoimbwa na Noorah? Ni nyimbo nzuri
iliyotamba miaka iliyopita na kuvuma zaidi baada ya video yake kutoka
ambapo ndani yake kulikuwa na Video queen aliyefahamika kwa jina la
Doreen.
Taarifa zilianza kusambaa kuwa mwanadada huyo kwa sasa ametumbukia
katika tatizo la matumizi ya dawa za kulevya huku akihitaji msaada
mkubwa.
Kupita ukurasa wa Instagram mwanamuziki Ray C ambaye nae aliwahi
kukumbwa na tatizo hilo akiweka picha yake pamoja na Doreen huku akidai
kuwa amempata na amekubali kuanza matibabu kuachana na dawa za kulevya.
Ray C ameandika kupitia Instagram >>> ‘Mungu ni mwema
sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasisi yangu ya
kuelimisha jamii kuhusu athari za dawa za kulevya nilipata emails nyingi
kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah
iitwayo ice cream!!nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye
website ya vibe magazine’.
‘Roho iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!! namshukuru
Mungu asubuhi ya juzi nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake
Doreen kichwa cha habari kikiwa msaada, nilipoisoma chozi lilinitoka
nika reply mara moja nilimuomba anitumie namba yake tuongee nikampigia
akaniambia doren hali yake si nzuri kutokana na drugs’
‘Moyoni nikawa nafikiria huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo
wake !!!!!ikawa Kama bahati tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia
tukutane kitengo cha dawa Mwananyamala! nilipomuona Doren kwa mara ya
kwanza nilifurahi kupita maelezo ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari
wake wa kuanza tiba ya methadone, isije ikawa amelazimishwa kuja
akaniambia dada yangu nimechoka maisha ya utumwa nisaidie!!’
‘Hicho ndo nilichotaka kusikia nikamwambia kwa uwezo wa Mungu Shetani
ameshindwa!!!!!! am soooo happy Doren ameanza tiba ya
Methadone!!!wapenzi wote wa bongoflava nawaomba tumwombee mdogo wetu
aweze kusimama kwenye tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwa
amani bila utumwa wa shetani’
‘God We Trust!!!I love You my lil’ sister….. nawahamasisha wengine huko
mliko mwenye ndugu, jamaa au rafiki njoo katika taasisi yetu uweze
kusaidiwa! usikubali maisha ya utumwa wa dawa za kulevya, njoo
tukusaidie… Ray C Foundation pamoja na kitengo cha Methadone We love you
guys, We can help you….”
No comments:
Post a Comment