Bondia Mada Maugo kushoto akiwa anapigana na Thomas Mahali mwenye rasta
Bondia Mada Maugo akiwa anazipanga kavukavu na bondia Thomas Mashali walipiokutana katika ukumbi wa Frends Corner Manzese
Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ubingwa wa UBO umekosa
kutangazwa mshindi mbele ya mashabiki baada ya vurugu kubwa kutokea
katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita
ubingwa huo uliokuwa ukigombaniwa na
mabondia Said Mbelwa na Karama Nyilawila alishindikana kupatikana
mshindi baada ya raundi ya nane bondia Karama kumpiga kichwa Mbelwa cha
wazawazi na kusababisha Mbelwa kuamaki kwa kulipiza kisasi na kumsukuma
nje pia kumrukia kama ninja wakati alipotoka nje ya uwanja mpambano huo
wa raundi kumi ulijikuta ukishia kwa raundi nane
na refarii pamoja na majaji wake
kukimbia ukumbini wakiwaacha mashabiki bila kureta majibu ya mpambano
huo hata hivyo mbelwa alirudi uringoni kwa ajili ya kuenderea kupambana
na mpinzani waka alikimbia moja kwa moja kutokana na kuona kihama cha
ngumi za mtaani zilivyuoanza
wakati huohuo bondia Mada Maugo alimpiga mwenzake Thomas Mashali kwa ngumi tatu mfululizo kavuvu
bila kufata sheria ambapo ni kinyume
na taratibu za mchezo wa masumbwi duniani kote mabondia hawo ambao wote
walionekana wamelewa walipishana kiswahili mbele ya promota Ally Mwazoa
ambaye ame haidi kabla ya kumaliza mwaka mabondia hawo wawe wameshapanda
uringoni
ambapo mpambano wao wa kwanza Thomas Mashali alimgalagaza kwa point Mada Maugo
katika mapambano ya utangulizi
yaliyochezwa siku hiyo bondia Khalid Chokoraa ambaye ni mwanamuziki
alimpiga kwa k,o ya raundi ya kwanza Abdul Manyenza na Mwaite juma
alimpiga Athumani Rashid wa Tanga kwa point wakati Selemani Galile
alipigwa kwa point na Abdalah Pazi
No comments:
Post a Comment