Kamati
ya Nidhamu, Rufaa na Usuluhishi ya Baraza la michezo la Taifa baada ya
kupitia, kuchambua na kumhoji kiongozi wa mchezo wa JUDO Ndugu Shabani
Kashinde Bundala, ambaye alikuwa katibu Mkuu wa Chama hicho kuhusu
tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa watu nje ya nchi kwa kisingizio
kuwa ni wanamichezo ambao wanakwenda kushiriki mashindano
yaliyoandaliwa huko, imeridhika na yaliyobainika katika sakata hilo bila
shaka yoyote ile na hivyo:-
Kamati inamfungia
maisha aliyekua katibu mkuu wa Chama cha JUDO Tanzania Ndugu Shabani
Kashinde Bundala kujihusisha na mchezo wa JUDO kama Kiongozi kuanzia
Tarehe 03 Machi, 2012. Aidha Bwana kashinde Shabani Bundala anafungiwa
maisha kujihusisha na maswala ya michezo kwa ujumla kwa sababu
zifuatazo:-
Bwana
Kashinde Shabani Bundala amebainika kujihusisha na mipango ya
kusafirisha watu nje ya nchi kwa kisingizio kuwa ni wanamichezo
wanakwenda kushiriki katika michezo iliyoandaliwa huko bila kibali wala
ruksa kutoka Baraza la Michezo la Taifa, huku akitambua wazi kuwa hilo
ni kosa na amefanya hivyo kama ifuatavyo:-
Mapema
mwaka 2011 alisafirisha watu wapatao 27 akiwemo nay eye mwenyewe mpaka
Nairobi kwenda kuomba Viza ubalozi wa Poland. Watu hawa baadhi
walinyimwa Viza kwa maelezo kuwa nyaraka zilizowasilishwa katika ubalozi
huo zilikuwa bandia na hivyo kusababisha ubalozi kuwasiliana
na Serikali juu ya uhalali wa shughuli za Ndugu Kashinde na timu yake.
Hata hivyo ilibainika wazi kuwa Baraza la Michezo la Taifa
haikifahamishwa juu ya safari hiyo ya wanajudo nje ya nchi.
Mwezi
Oktoba, 2011, Ndugu Kashinde aliwasilisha orodha ya majina ya watu kumi
na nane (18) katika ubalozi wa Ufaransa. Hata hivyo baada ya Maafisa wa
Ubalozi kuchambua majina na nyaraka husika walibaini kuwa nyaraka zao
nyingi zilikuwa batili na za kugushi. Ubalozi wa ufaransa ulifanya
mawasiliano na Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ambao
nao waliwasiliana na Wizara husika na hatimaye Baraza la Michezo, hata
hivyo ilibainika wazi kuwa hakuna taarifa iliyokuwa imetolewa na chama
cha JUDO kwa Serikali juu ya afari hiyo. Hivyo haikuwa na kibali kutoka
Serikalini.
Aidha
kwa kua suala zima la ndugu Kashinde linaonekana kuwa ni la makosa ya
jinai, Baraza la Michezo la Taifa halijui kuna nini nyuma ya Jeshi la
Polisi kwa uchunguzi na hatua zaidi kadri ya taratibu zao.
Aidha,
tunapenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa Watanzania wote wenye
mapenzi mema na michezo wa JUDO kugombea uongozi katika mchezo huo ambao
uko wa kutokana na Viongozi waliokuwepo kumaliza muda wao.
Baraza
la Michezo la Taifa linaomba kutoa tahadhari kuwa kuanzia sasa
Wanamichezo wote watakaotaka kusafiri nje ya nchi iwe timu au mtu mmoja
mmoja lazima wapeleke taarifa Baraza la Michezo la Taifa siku 14 kabla
ya safari yao ili wapewe kibali kama Sheria ya Baraza lamichezo la Taifa
inavyotaka.
No comments:
Post a Comment