Pia
kwaya mahiri ya Kinondoni Revival inayotamba na albamu yao mpya ya Mtu
wa Nne, inatarajia kutumbuiza katika tamasha la Pasaka na Mwinjilisti
Faraja Ntaboba kutoka DRC.
Mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe. Baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa,
mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9
mwaka huu.
"Katika
tamasha la Pasaka mwaka huu, Rebecca Malope atapata fursa ya kuimba
nyimbo mbalimbali zilizomo kwenye albamu zake," alisema Msama.
Rebecca
amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009),
Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at
Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits
(Januari 10, 2006).
"Bado
tunaendelea na mazungumzo na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa
Injili, lakini Rebecca atakuwepo akishirikiana na wengine mahiri kama
Rose Muhando, Solomon Mukubwa na wengineo," alisema Msama.
Tamasha
la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya
kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.
Kiingilio
katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh.
2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh.
10,000.
Rebecca Malope ni mwimbaji nguli wa Afrika Kusini aliyetamba zaidi kimataifa mwishoni mwa miaka ya 90.
Malope alizaliwa katika shamba la tumbaku Afrika Kusini. Akiwa mtoto, yeye na dada zake walikuwa wakiimba kwaya kanisani.
Alijiunga na kundi la muziki wa injili akiwa binti mwenye umri mdogo, jijini Johannesburg, chini ya mtozi, Zizwe Zakho.
Alianza
kutoa albamu yake ya kwanza aliyoipeleka Marekani mwaka 1996 na mwaka
uliofuata alisaini mkataba na EMI kisha akatoa albamu ya Free At Last
No comments:
Post a Comment