Warembo
watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata
2012, watatambulishwa Jumapili ya Pasaka Aprili 8 katika ukumbi wa Dar Wes Park,
Tabata.
Mratibu wa
shindano hilo Joseph Kapinga amesema jana kuwa mashabiki wa urembo watapata
fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla ya kushiriki kwenye shindano la
Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa Mei.
Kapinga amesema
utambulisho huo utasindikizwa na burudani mbalimbali ikijumuisha muziki wa
dansi, taarab, bongo fleva na muziki wa asili.
Mratibu huyo
alisema warembo wanaotaka kushiriki kwenye shindano la Miss Tabata wanatakiwa
kuripoti katika ukumbi wa Dar West Park Tabata kuanzia saa nane mchana kwa ajili
ya kujiandaa na maandalizi ya Miss Tabata.
Kapinga alisema
warembo 13 wameshajitokeza kushiriki Miss Tabata. Warembo hao ni
Neema Saleh Kazumari (18), Paulina Valentine (18), Khadija Nurdin
(19), Phillos Lemi (20) na Mercy Mlay (21).
Wengine ni
Neema Innocent (19), Ellen Sule (22), Wikllihemina
Mvungi (20), Queen Issa (20), Suzane Deodatus (19), Everline Andrew (21),
Josephine Peter (20) na Jamila Omary (19). Warembo hao wako chini
ya wakufunzi watatu- Beatrice Joseph, Neema Chaki na Bokilo Junior.
Zaidi ya warembo 10 kutoka Tabata watafuzu
kushiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye
mwaka huu.
Mrembo
anayeshikilia taji la Tabata ni Faiza Ally.
Warembo wa
Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka
juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi
wa kinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka juzi Julliet William pia
alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
Miss Tabata
inaandaliwa na Boob Entertainment na Keen Arts.
No comments:
Post a Comment