MAANDALIZI
kwa ajili ya bonanza la vyombo mbalimbali vya habari litakalofanyika
Machi 24 mwaka huu ukumbi wa Msasani Beach Club, Dar es Salaam
yanaendelea vizuri.
Tayari
Kamati ya Maandalizi imeshatuma barua za mialiko kwa vyombo mbalimbali
vya habari na naomba wote walialikwa wathibitishe haraka iwezekanavyo
ushiriki wao kulingana na walivyojulishwa.
Pia
Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA), imeshafanya maandalizi ya burudani mbalimbali kwa ajili ya
bonanza hilo, ikiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, ambao bado
tunaendelea na mazungumzo nao.
Tayari
kamati imeshamalizana na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’
kutumbuiza kwenye bonanza hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL).
Hivyo
burudani itakuwa Wazee wa Ngwasuma na wasanii wa muziki wa kizazi
kipya, ambao tutawatambulisha siku yoyote wiki hii kabla ya Alhamisi
pamoja na mgeni rasmi.
Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia burudani, michezo na mambo mengine yawe ya aina yake.
Bonanza
litaanza saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku, ambapo baadhi ya
michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za
magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na
michezo.
Tunaonya
kuwa kampuni ambayo itashindwa kuthibitisha ushiriki wake mapema kwa
michezo itakayocheza haitapangwa, hivyo tunaomba wahusika watilie mkazo
jambo hilo.
No comments:
Post a Comment