Watu watano wanaotuhumiwa kumuimbia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, wametiwa mbaroni baada ya kukamatwa usiku wa kuamkia jana katika Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro.
Baadhi ya vitu alivyoibiwa Malima ikiwemo simu na kompyuta mbili vimepatikana katika maeneo ya Kata ya Kichangani na Mafiga.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro, Hamis Seleman, alisema watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Chamwino walikamatwa usiku wa kuamkia jana.
Alidai kuwa vijana hao baada ya kuwibia Malima, vifaa mbalimbali zikiwemo dola za Marekani 4,000 walienda kuzibadilisha dola hizo katika duka la kubadilisha fedha za kigeni eneo la Posta na kupata Shilingi ya Tanzania na kugawana.
Inatajwa kuwa watuhumiwa hao baada ya kuiba simu hizo, walishindwa kuziuza kwa kuwa zilikuwa na picha ya Malima akiwa na mwanawe ambayo walishindwa kuiondoa.
No comments:
Post a Comment