Wanafunzi
60 wa jinsi ya Kiume wa Shule ya Sekondari Simbega Kata ya Iyula,
Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya lori walilokuwa
wakisafiria, kutoka Kijiji cha Ruanda wilayani humo kuacha njia na
kisha kupinduka.
Ajali
hiyo imeyokea mita chache baada ya kupanda lori hilo, ambapo,
wanafunzi wenzao wa jinsi ya kike kutangulia na lori jingine wakitokea
mchezoni baada ya dereva wa lori hilo Bwana Juhudi Shonde kushindwa
kulimudu gari hilo wakati likipanda mlima ndipo alipoamua kuruka na
kuliacha gari hilo likirudi nyumba na kisha kupinduka likiwa na
wanafunzi ndani.
Tukio
hilo limetokea majira ya saa 3 usiku Februari 16, ambapo kati ya
wanafunzi 60 waliokuwemo 37 na mwalimu mmoja wamejeruhiwa na kukimbizwa
katika Hospitali ya Serikali Mbozi na wanafunzi wanane na mwalimu mmoja
wamelazwa katika Hospitali ya Ifisi, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Miongoni
mwa majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mbozi wawili hali zao ni
mbaya kutokana na kuvunjika miguu na Daktari wa zamu aliowapokea
amewataja kuwa ni pamoja na Bahati Mwashambwa na Ajuaye Shonde na wliopo
Hospitali ya Ifisi ni Mwalimu Enock Mabula ambaye ameumia goti na
kupata majeraha.
Kwa
upande wake Mkuu wa Shule hiyo Bwana Jacob Nsenye, amesema wazazi wa
wanafunzi hao wasiwe na hofu hali zao zinaendelea vema kwa mujibu wa
daktari.
No comments:
Post a Comment