Rais wa Riadha Tanzania (RT), Francis John akizungumza wakati wa utambuilisho wa mbio za Tabora Marathon.
KAMATI
ya mbio za Tabora Marathon 2012, leo inatarajiwa kuanika zawadi za
washindi wa mbio hizo za kwanza kihistoria kufanyika mkoani humo.
Mbio
za Tabora Marathon 2012 zinatarajiwa kurindima mjini Tabora Machi 10
na kushirikisha wakimbiaji kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya
Magharibi.
Kwa
mujibu wa Mshauri wa Ufundi wa Tabora Marathon, Tullo Chambo, leo
watafanya jukumu hilo baada ya kufanikiwa kukamilisha maandalizi
mbalimbali, ikiwamo wadhamini.
Chambo
alisema, licha ya ugumu wa upatikanaji wa wadhamini, lakini
wanawashukuru waliojitokeza kufanikisha mbio hizo, ambazo ni chachu ya
kuhamasisha mchezo huo na kuibua vipaji.
“Kimsingi
hadi kufikia hatua hii, tumehangaika usiku na mchana na ninawashukuru
wapenda michezo wote walionyesha mapenzi mema na mchezo huu na Mkoa wa
Tabora kwa ujumla, kwa kuweza kufanikisha kufanyika kwa mashindano haya
ya kipekee katika historia ya mchezo wa riadha mkoani Tabora na Kanda
ya Magharibi kwa ujumla,” alisema Chambo na kuongeza kuwa;
Leo
tutawaanika wote waliofanikisha mbio hizi katika mazingira magumu,
pamoja na zawadi ambazo washindi watazawadiwa katika mbio hizo.
Pia
aliwapongeza viongozi wa serikali mkoani Tabora, chini ya RC, Fatma
Mwasa, na viongozi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Tabora, kwa ushirikiano
wao uliofanikisha kufikia hatua hii.
No comments:
Post a Comment