Watu
wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira
kali katika Kijiji cha Myunga, Wilaya ya Momba (Jimbo la Mbozi
Magharibi) mkoani Mbeya.
Majambazi
hayo yameuawa usiku wa manane yalipokwenda katika kijiji hicho kwa nia
ya kutekeleza mauaji kwa diwani wa Kata ya Myunga (CHADEMA) mheshimiwa
Godfrey Siame, ambapo waliahidiwa kupewa milioni mbili.
Majambazi
hayo yakiwa na silaha mbili aina ya shortgan na bastola walipofika
kijijini hapo na kisha kumrubuni Diwani huyo kuwa wanataka kudanya naye
biashara, ndipo aliwashitukia kuwa ni majambazi wakati yeye akiwa
Tunduma baada ya mtego wakati wakitoka katika nyumba moja ya kulala
wageni kwa ajili ya kutekeleza azma yao walikamatwa na wananchi wenye
hasira kali na kuanza kupingwa hadi kuuawa.
Wakati
huohuo usiku wa kuamia jana mahabusu wanne waliokuwa katika mahabusu ya
polisi Kituo Kikuu cha Kati Mbeya wametoroka baada ya kufanikiwa
kuchimba ukuta wa vyumba vya mahabusu bila Askari waliokuwa zamu kujua.
Askari
hao walifanya ukaguzi majira ya saa nane usiku saa tisa usiku wakabaini
mahabusu hao hawapo baada ya kuchimba moja ya ukuta kisha kutokomea
gizani na kuwaacha Polisi wakiwa katika lindo.
Mbinu
iliyotumika ni kuloanisha ukuta kwa kutumia maji yaliyopo bafuni na
vipande viwili vya nondo ambavyo walivitumia kuuchimba ukuta huo kwa
urahisi licha ya kujengwa kwa matofari ya saruji.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea
kwa matukio yote wawili na kwamba mahabusu watatu walikuwa wanakabilisha
na kesi za mauaji na mmoja kesi ya wizi.
Hata
hivyo amesema Jeshi lake limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye
ni Fadhili Mwaitebele (27), mkazi wa Ilomba jijini Mbeya ambaye alikuwa
anatuhumiwa kwa wizi.
No comments:
Post a Comment