Mechi
kati ya Kombe la FA kati ya Tottenham na Bolton Wanderers ilisimamishwa
ghafula baada ya mchezaji wa Bolton, Fabrice Muamba kuzimia ghafula, na
kushindwa kuvuta pumzi.Madaktari
walijaribu kwa dakika 10 kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23
aweze kupumua, na hilo liliposhindikana, ilimlazimu mwamuzi Howard Webb
kusimamisha mchezo wakati ukiwa 1-1 katika dakika ya 41. Muamba
alizaliwa tarehe 6 Aprili mwaka 1988 mjini Kinshasa, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo, na aliimarika kisoka katika chuo cha vijana wadogo
cha Arsenal, na akiiwakilisha England katika mechi mbalimbali, tangu
zile za vijana wa miaka 16, hadi zile za wale wa miaka 21. Alijiunga na
Birmingham mwaka 2007, na kuhamia Bolton mwaka uliofuata.
No comments:
Post a Comment