Moto mkubwa ambao chanzo chake bado
kufahamika umeteketeza vyumba viwili vya bweni la wasichana maarufu
kama Hall 6 vyumba Block W katika chuo kikuu kishiriki cha elimu
Mkwawa (MUCE) Iringa .
Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza
mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha moto huo
bado hakifahamiki .
Walisema kuwa moto huo ulianza
kuwaka katika chumba kimoja wapo chumba Block W muda wa saa 6 mchana
na kuwa wakati huo baadhi ya wanafunzi walikuwa wamejipumzisha
katika vyumba hivyo .
Hivyo walisema kuwa waliona moto
huo ukianza kuwaka katika chumba kimoja wapo na kuanza jitihada za
kujaribu kuzima moto huo bila mafanikio hadi kikosi cha zimatomo
kutoka Manispaa ya Iringa na jeshi la polisi walipofika kuzima moto
huo.
Mkuu wa chuo hicho cha Mkwawa
Prof. Philimon Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la moto
japo amesema kwa sasa ni mapema sana kuelezea kwa kina suala hilo
na kuwa taarifa zaidi ataitoa baada ya uchunguzi wa tukio hilo
kufahamika ikiwa ni pamoja na kujua madhara yaliyojitokeza na chanzo
cha moto huo.
Uchunguzi wa mtandao huu umebaini kuwa moto huo umeanza kuwaka
katika moja kati ya soketi za umeme katika chumba hicho hali
inayoonyesha kuwa yawezekana watumiaji wa chumba hicho walikuwa
wakitumia hita ama pasi
No comments:
Post a Comment