Mwanamitindo
wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese ataendesha zoezi la
kutafuta wanamitindo wawili (kwa vijana wa kike na kiume) watakoshiriki
kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya wiki ya Mavazi ya Afrika
Kusini (South Africa Fashion Week) tarehe 1 April mwaka huu.
Millen
atafanya zoezi hilo kupitia kampuni yake ijulikanayo kwa jina la
Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza
Tanzania kupitia fani ya mitindo (Tanzania International Fashion Exposé
(TIFEX).
Alisema
kuwa wanamitindo wanaotaka kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania
katika SAFW kufika siku ya Jumapili tarehe 25 mwezi huu kwa ajili ya
mchujo huo kuanzia saa 8.00 mchana kwenye hotel ya Serena.
Alifafanua
kuwa anaamini kuwa wanamitindo wa Tanzania watakaopatikana katika
zoezi hilo wataiwakilisha Tanzania vyema katika wiki ya maonyesho ya
mavazi ya Afrika Kusini na kuitangaza Tanzania kimataifa kama
anavyofanya yeye kwa hivi sasa.
Alisema kuwa hiyo ni fursa pekee kwa wanamitindo kuweza kujitangaza wenyewe kimataifa na kufuata nyayo zake.
Alifafanua
kuwa wanamitindo wanaotakiwa kufika katika zoezi lazima wawe na vigezo
vifuatavyo:- Umri miaka 18 mpaka 24, urefu 1. 75m, hips 37cm (ukiwa na
nywele zako za asili) na kwa wanaume urefu ni 1.82m.
“Naamini
kuwa zoezi hili litawanufaisha wana mitindo wa kike na wa kiume wa
Tanzania na vile vile ushiriki wao katika SAFW na katika maonyesho
mengine ya mavazi nje ya Afrika na kusaidia kuitangaza nchi kimataifa,”
alisema Millen.
Alisema
kuwa lengo kubwa la kampuni yake ni kuendeleza fani ya uanamitindo na
vile vile kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake kwa kupitia fani ya
mitindo na hata kwa njia ya utalii.
Aliongeza
kuwa japo Tanzania ina wanamitindo wengi na wabunifu, bado kuna pengo
kubwa ukilinganisha na maendeleo ya fani hiyo katika nchi ya Afrika
Kusini na Nigeria.
Alisema
kuwa nchi hizo zimepiga hatua kubwa sana na yeye kuhamasika kuanzisha
kampuni yake iliyozinduliwa mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuziba
pengo hilo na kuleta maendeleo ili wahusika wafaidike na matunda ya
fani yao.
Majaji wa zoezi hilo ni Ritha
Poulsen, Mustapha Hassanali na Khadija Mwanamboka na katika kuwekea
umuhimu zaidi mchakato huo, MMG imemkaribisha mwanamitindo maarufu,
Aminat Ayinde kutoka America Next top model cycle 12 kushuhudia zoezi
hilo.
No comments:
Post a Comment