DK. HARRISON MWAKYEMBE AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKELEO
Nauibu
Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akiazungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake jijini Dar es salaam leo, kuhusu maendeleo ya
afya yake baada ya kurejea nchini ambapo amesema kuwa kwa hivi sasa
anaendelea vizuri na kwamba yupo fiti kiafya, na tayari ameripoti
ofisini rasmi leo kwa kuanza kazi. Mwakyembe hakutaka kuweka wazi
kuhusu mambo mengine aliyokuwa akiulizwa na waandishi wa habari kuhusu
uvumi ulioenea juu ya afya yake na kusema mambo yote anaiachia serikali
kupitia tume maalumu iliyoundwa kufutilia suala la ugonjwa wake.
No comments:
Post a Comment