Mbunge
wa Njombe Kusini na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda
akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika kijiji cha Idundilanga.
Baada
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
kutangaza nia ya kuugawa mkoa wa Iringa ili kuwa na mikoa miwili yaani
mkoa wa Iringa na Mkoa wa Njombe, wananchi wa mkoa mpya wa Njombe
hawalali hadi kieleweke. Kwa kujituma kunakostahili kuwa mfano wa kuigwa
na kwa ushirikiano usiojali imani, kabila au itikadi za kisiasa
wamedhamiria kuujenga mkoa wao huo kwa kiwango cha hali ya juu.
Mbinu wanazotumia ni kupiga vita umaskini kwa kuchapa kazi hususan za
kilimo cha mazao ya chakula (mahindi, matunda, viazi,) na biashara
(miti ya mbao), kupiga vita ujinga kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa
na shule ya awali na msingi pamoja na kila kata kuwa na shule ya
upili, na kupiga vita maradhi kwa kujenga zahanati na vituo vya afya.
Wakionesha ari na msukumo mkubwa kwa Mbunge wao Mhe. Anne
Semamba Makinda aliyewatembelea wananchi hao hivi karibuni, wananchi
hao wanajivunia tabia yao ya kupenda kufanya kazi kwa bidii na
kujituma, ardhi yenye rutuba walio nayo pamoja na ukanda wanamoishi wa
nyanda za juu kusini wenye mvua za kutosha nyakati zote.
Akizungumza
nao mbunge huyo aliwasisitizia kujipanga vizuri ili kuzifaidi fursa
zitakazotokana na uchimbaji wa mkaa wa mawe pamoja na chuma katika
migodi ya Ludewa na Liganga ambayo utekelezaji wake tayari uko katika
hatua za kuanza uchimbaji. Zifuatazo ni baadhi ya shughuli ambazo
wananchi wa Njombe wanashiriki. (Prosper Minja)
No comments:
Post a Comment