Waziri
wa Afya Dr Haji Mponda amesema yeye atajiuzulu ili kuokoa roho za
watanzania ambao wataathirika na mgomo mpya wa madaktari na si kwa
shinikizo la madaktari hao! Hayo aliyasema jana usiku kwenye kikao cha
dharura cha baraza la Mawaziri cha kujadili mgomo mpya wa Madaktari na
Manesi! Hata hivyo Mponda ametoa rai kwamba watanzania wawe makini sana
na jinsi watu wanavyotumia migogoro kwa maslahi yao binafsi huku
wakisababisha maafa makubwa kwa raia wasio na hatia, pia aliongeza kwa
kusema kuwa kama wanataaluma wataingia kwenye ushabiki wa siasa nchi
itaingia kwenye mgogoro mkubwa na kudhoofisha ustawi wa taifa letu!
No comments:
Post a Comment