STAA wa Filamu na Maigizo Bongo, ambaye kwasasa anachapa mzingo Kwenye kipindi cha Hatua Tatu kinachorushwa hewani kupitia 100.5 Times FM, Sintah Manongi 'Sintah JLO Africa', juzikati alifyatuka kwakusema kuwa anahitaji bwana wa kuzaa naye maana amezidi kusema kila kona na ndugu na marafiki zake wa karibu.
Akigonga stori mbili tatu na mwandishi wa habari hizi, Machi 27 mwaka huu Sintah alisema kuwa, amefikia kusema hivyo kwakua tayari umefikia wakati wake wa kuitwa mama maana siku zinazidi kwenda mbele na akisema asubiri ndoa ndiyo azae bado itazidi kumchukua muda mrefu kumpata atakayeendana naye kitabia kama ndoto zake zilivyo siku zote.
"Niko
Sileas na hili na wala sitanii tena maana sasa nimezidi kukoseshwa raha
na marafiki zangu kila mmoja ukiongea naye habari zinazohusiana na
mtoto basi utasikia ananisema tena wakati huo anakuwa hatanii hata
kidogo, sasa kuepusha maneno nitazaa pale tu nitakapopata mwanaume wa
kuzaa naye, alisema Sintah a.k.a JLO Africa
No comments:
Post a Comment