PRESS RELEASE
KUWEPO KWA VIKUNDI VYA WANENGUAJI NA BENDI ZINAZOKIUKA
MAADILI YA KITANZANIA
Katika siku za
karibuni kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili kupitia maonyesho ya
majukwaani na kazi mbalimbali za Sanaa.
Kutokana na hali hii, Baraza la Sanaa la
Taifa kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa Jumatatu ya Tarehe 26/03/2012 litakuwa
na mada maalum ya Unenguaji na Maleba Katika Muziki.
Mada hii itakayowasilishwa na Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) na asasi ya Sanaa ya Binti Leo pamoja na mambo mengine
itaangalia hali halisi ya Sanaa ya unenguaji, maleba na matatizo yaliyopo na
hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
BASATA inatoa wito kwa wadau wote wa Sanaa
na wapenzi wa Utamaduni wan nchi yetu kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushiriki
kuchangia mwelekeo mpya wenye maadili sahihi ya kitanzania.
Sanaa ni Kazi Kwa
Pamoja Tuikuze na Kuithamini.
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI, BASATA
No comments:
Post a Comment