Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa 
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amevipatia vukundi saba vya Vikoba 
vilivyopo Wilayani Monduli,kiasi cha shilingi milioni nane kwa ajili ya 
kuendeleza shughuli zao.Lowassa amesema yeye ni mkereketwa mkubwa wa 
Vikoba huku akisisitiza kuwa ni chachu ya maendeleo na kumkwamua 
mtanzania kutoka katika umasikini. kila kikundi kimepata shilingi 
millioni moja ambapo kikundi kilichofanya vizuri kimeongezewa shilingi 
millioni moja zaidi.Pichani ni Mh. Lowassa akikabidhiwa zawadi na 
mwenyekiti wa Vikoba Kijiji cha Monduli Juu,Dawson Kaaya wakati viongozi
 wa vikundi hivyo walipomtembelea nyumbani kwake Monduli.
Mmoja wa viongozi wa vikundi vya vikoba Kijiji cha Monduli Mjini akisoma risala mbele ya Mh Lowassa.
Baadhi ya wanavikoba wa Monduli Mjini wakimsikiliza Mh. Lowassa.
Mhe Edward Lowassa akipewa zawadi na 
Bi Arafa Ismaild kutoka katika vikundi vya Vikoba Monduli mjini ambao 
walikwenda kumtembelea nyumbani kwake. Kushoto kwa Mh.Lowassa ni Bw. 
Dawson Kaaya ambaye ni Mwenyekiti wa Vikoba Monduli Mjini.
 
 
No comments:
Post a Comment