Waasi
 nchini Syria wamewaachia huru raia 50 wa Iran waliowakamata mwaka 
uliopita, kwa masharti la kubadilisha na zaidi ya raia 2000 
wanaoshikiliwa na serikali ya Rais Bashar al Assad. 
Raia
 48 wa Iran wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la Islamic Revolutionary
 Guard Corps waliotumwa kupigana upande wa serikali wameonekana katika 
hotel mjini Damascus wakiwa katika hali nzuri kiafya.
 Iran,
 mshirika wa karibu wa serikali ya Assad, alisema kuwa watu hao ni 
mahujaji wa madhehebu ya Shia waliokuja nchini Syria kufanya ibada 
katika maeneo tukufu. 
Wakati
 huohuo, Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za 
Kiarabu kwenye mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi yuko mbioni  kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa Marekani na Urusi mjini Geneva kesho Ijumaa.
Mkutano 
huu unafanyika ikiwa ni siku kadhaa baada ya Rais Assad kutoa hotuba 
yake ambayo ilitaka kuwepo kwa majadiliano ya amani yatakayomaliza 
machafuko nchini humo. Hata hivyo Jumatano iliyopita bwana Brahimi 
aliita hotuba hiyo ya Assad kuwa ni ya kidini na yenye kupendelea upande
 mmoja.
 
 

No comments:
Post a Comment