| BAADA ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko. | 
| 
 
Mara
 baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende 
kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu 
yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na 
kuumia wengine walipoteza fahamu.  
Hata
 hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano 
huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo 
la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa 
watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu. | 
 
 
No comments:
Post a Comment