Kwa mujibu wa gazeti la The Star ka nchini Kenya, rapper Joseph Haule
 aka r Profesa Jay hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro na promoter wa 
mjini Mombasa Kenya aliyemchukua kufanya show. Prof alikuwa amechukuliwa
 kufanya show mbili siku ya Christmas kwenye kumbi za Jamboree Resort na
 Quetu Beach Resort.
 Inavyodaiwa  Profesa Jay hakuwa amelipwa fedha zote kwa show ya pili 
na hivyo alipewa camera aina ya  Nikon D3000 kama rehani.Baada ya show, 
Prof aliondoka nchini Kenya na crew yake na kuibeba kamera hiyo. Sasa 
waandaaji hao wanadai kuwa walimpatia Prof hela yake iliyokuwa imesalia.
 Issue hiyo imekuwa kubwa kiasi ambacho passport ya mpambe aliyekuwa 
amesafiri na Jay nchini humo imeshikiliwa ili asiondoke.Waandaaji 
wanadai kuwa walimlipa Profesa Jay shilingi 252,000 za Kenya ambazo ni 
zaidi hata ya fedha walizokuwa wamekubaliana na sasa wanataka 
warudishiwe fedha yao.
Polisi wanashughulikia kesi hiyo na Prof aliyekuwa ameingia 
makubaliano ya show nyingine katika ukumbi wa Jamboree December 31 
aliitosa show hiyo.source na gumzo la jiji
 
 

No comments:
Post a Comment