Mwansidhi wa Habari wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Issa Ngumba (45) enzi za uhai wake.
 MWANDISHI
 wa Habari wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko, Mkoa wa Kigoma, 
Issa Ngumba (45), ameuawa kwa kupigwa risasi na kunyongwa na watu 
wasiofahamika.
Habari
 zilizopatikana jana zimeeleza kuwa mwili wa mwandishi huyo ulikutwa 
porini, siku tatu tangu alipotoweka nyumbani kwake katika mazingira ya 
kutatanisha.
Kamanda
 wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai alithibitisha tukio hilo, 
lakini akasema asingeweza kulizungumzia kwa undani kwa kuwa polisi 
walikuwa bado eneo la tukio.
Baadhi
 ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwandishi huyo alikutwa jana akiwa 
amekufa, huku mwili wake ukiwa na majeraha ya risasi na ukiwa umenyongwa
 na pembeni yake kulikuwa bastola iliyokuwa imetelekezwa pamoja na simu 
zake mbili za mkononi.
“Mwili
 wake ulipatikana jana katika Pori la Mlima Kajuluheta ulioko katika 
Kijiji cha Muhange, Kakonko asubuhi baada ya wananchi kufanya msako wa 
siku tatu tangu Jumapili iliyopita ikiwa ni siku moja baada ya kupotea 
katika mazingira ya kutatanisha,” alisema mmoja wa  mashuhuda hao.
Imeelezwa
 kuwa pamoja  na vifaa hivyo, pia katika eneo hilo la tukio kulikutwa 
risasi tano na katika mfuko mmoja wa suruali ya marehemu, kulikuwa na 
noti moja ya Sh10,000.
Mwenyekiti
 wa Klabu ya Waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deogratius Nsokolo 
alisema: “Sisi ndiyo kwanza tunaelekea eneo la tukio, lakini waandishi 
wa Wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia 
uchunguzi wa daktari, wameeleza kuwa marehemu amekufa kwa kunyongwa na 
kupigwa risasi mkono wa kushoto.”
“Tunaelekea
 Wilaya ya Kakonko kutoka Kigoma Mjini, lakini daktari amesema maiti 
inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa risasi mkononi.”
Alisema mwili huo ulifanyiwa uchunguzi na daktari Primus Ijumaa wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.
Kamanda
 Kashai alisema jeshi lake linasubiri taarifa ya daktari aliyefanya 
uchunguzi wa mwili wa marehemu pamoja na taarifa za awali za uchunguzi 
kabla ya kutoa taarifa kamili kwa waandishi wa habari.
Naibu
 Mhariri wa Kituo cha Redio Kwizera kinachorusha matangazo yake kutoka 
wilayani Ngara mkoani Kagera, Seifu Upupu alisema mwandishi huyo 
alipotea tangu Januari 5, mwaka huu saa kumi na moja jioni.
“Simu
 zake zilikuwa zikiita bila kupokewa kwa muda wote na hadi jana (juzi) 
zikawa hazipatikani kabisa,’ alisema Upupu na kuongeza:
 
 

No comments:
Post a Comment