Pichani kati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba akipata maelezo mafupi kutoka kwa Rais wa  Shirikisho
 la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba (wa pili kushoto) kuhusiana
 na mikakati na mipango mbalimbali ya mazishi ya Marehemu Sadick Juma 
Kilowoko a.k.a Sajuki,nyumbani kwao Tabata Bima,jijini Dar.Aidha kwa 
taarifa rasmi kutoka kwa Simon Mwakifwamba ameeleza kuwa mazishi ya 
marehemu yatafanyika kwenye makaburi ya Kisutu siku ya Ijumaa mapema saa
 tano asubuhi.Kuli kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi wa utafiti wa Clouds 
Media Group,Ruge Mutahaba.

Rais wa  Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi
 na Teknolojia,Mh January Makamba kuhusiana na taratibu mbalimbali 
kuhusiana na msiba huo,huku baadhi ya wasanii wengine mahiri wa filamu 
wakisikiliza kwa makini.

 Mazungumzo
 mengine ya hapa na pale yakiendelea kufanyika kuhusiana taratibu nzima 
za msiba wa Sajuki,ulioko Tabata Bima,jijini Dar.
 
 

No comments:
Post a Comment