Baada ya kugundua wananchi wamemshtukia baada ya kumhoji maswali na 
kushindwa kujibu aliamua kutimua mbio kukwepa kamera ya Francis Godwin 
isimpate picha yake, kama unavyomuona hapo mdau mguu gafla umetokea 
kimiujiza pamoja na mkono, yote hiyo alikuwa ameificha kwa kutumia koti 
lake na Suruali alizovaa. 
Baada ya hali kuwa tete alijikuta anazisahaumpaka kandambili zake, kama unavyoziona. 
Huyu  ni omba omba anayeigiza  kutokuwa na mkono 
mmoja na mguu Mmoja akiwa amekaa eneo la M.R Iringa mjini akisubiri  kuomba chochote  kutoka kwa  
wapita njia leo.
Ule  usemi wa  wahenga  kuwa  ukistaajabu ya mussa utayaona ya 
firauni leo umetimia katika  eneo la M.R mjini Iringa baada ya  wananchi  
waliokuwepo eneo hilo kupigwa na butwaa baada ya mzee janja ambaye amekuwa 
akishinda eneo hilo na kujifanya mlemavu asiyekuwa na mkono mmoja na mguu  
mmoja kutimua mboni kukwepa kamera ya mtandao  huu.
Tukio  hilo limetokea 
majira ya saa 8 mchana baada ya camera ya mtandao huo  kufika  eneo  hilo la 
kushuhudia umati  wa wananchi  wakiendelea  kumpa  fedha mzee janja  huyo ambae 
alijifanya mlemavu  wa vuongo na kuongea kwa  shida .
Hata  hivyo baada 
ya mmoja kati ya  wananchi kufika  eneo hilo alionyesha  kufichua mbinu hiyo 
chafu ya  mzee  huyo kujifanya ni mlemavu  wakati asubuhi alikutana nae maeneo ya mjini akiwa 
mzima wa afya  njema na katika  kumhoji zaidi  ndipo kamera ya mtandao huu  
ilipoamua  kufanya kazi yake  ya kunasa  kituko  hicho na ndipo mzee   huyo 
alipoanza  kuongea  kwa  sauti vizuri  tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa 
hawezi kuongea kabisa (bubu)
Wakati mabishano yakiendelea  eneo hilo 
ghafla  mzee  huyo alisimama kwa miguu  yake  yote  miwili pamoja tofauti na  awali 
alivyokuwa akijifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya  watu  kutaka  apigwe  
picha ndipo mzee  huyo alipoanza  kutimua mbio  huku ulemavu aliokuwa nao 
akiusahau hapo  pamoja na kandambili zake na hakuna mtu  aliyeweza  kumfukuza na 
kufanikiwa  kumkuta.
Baadhi ya  wananchi  wameuomba uongozi  wa Manispaa 
ya Iringa  kuwabana  omba omba hao ambao  wamekuwa  wakidanganya  watu kuwa  wao 
ni  walemavu kumbe ni  wazima na kutaka  kuwepo kw
 
 
No comments:
Post a Comment