Miongoni mwa nyara za serekali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu kwenye nyumba ya mtuhumiwa Peter 
Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya
nchi.
********
Mahmoud Ahmad Arusha
JESHI la polisi mkoani 
Arusha,limekamata shehena kubwa ya nyara mbalimbali za serikali 
zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu,eneo la Matevesi Kisongo 
nje kidogo ya jiji la Arusha,zikiwa tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.
Nyara hizo ni pamoja na Ngozi za 
Simba,Chui na Mamba ,meno ya Tembo,vichwa vya Nyani,Swala na Nyati,Pembe
 za kifaru,na zingine nyingi ambazo jeshi la polisi linaendelea 
kuzitambua.
Sambamba na hilo jeshi hilo 
limemtia mbaroni mtuhumiwa wa nyara hizo aliyetambulika kwa jina la 
Peter Leurence (55)mkazi Ngaramtoni ya chini,ambaye alikuwa akiwa 
amezihifadhi kwenye maboksi zaidi ya 20,kwenye nyumba yake iliyopo eneo 
hilo.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi 
mkoni Arusha,Liberatus Sabas tukio la kukamatwa kwa nyara hizo limetokea
 jana majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo  eneo la kisongo mtaa wa 
mateves baada yak upata taarifa kutoka kwa raia wema.
Kamanda Sabas alisema kuwa baada 
ya jeshi hilo kupata taarifa za siri majira ya saa 5 asubuhi walifika 
eneo la tukio majira ya saa 7 mchana na kupata upinzani mkubwa kutoka 
kwa walinzi wa wanaolinda eneo hilo kwani waliwanyima kuwapa maelekezo 
ya kumpata mmiliki wa nyumba hiyo.
Hata hivyo alisema kwamba askari 
hao waliamua kumueka chini ya ulinzi kwa kumshurutisha mlinzi mmoja 
iliaweze kuwapa ushirikiano ambapo aliwapaita namba za simu na mtuhumiwa
 aliwaambia kuwa yupo magugu mkoani Manyara na angefika saa 12 majira ya
 jioni.
Taarifa zinadai kuwa baada ya 
mtuhumiwa kufika jitihada za kufanya upekuzi zilifanyika chini ya polisi
 wenye silaha za moto na walikuta shehena kubwa ya nyara za serekali 
zilizokuwa zimahifadhiwa kwenye ghala maalum na kufungwa kwenye mabox 
 teyari kusafirishwa kwenda kusikojulikana.
Alisema kuwa polisi waliamua 
kuweka ulinzi hadi kulipokucha na huku wakiendelea kumshikilia mtuhumiwa
 huyo  na jeshi hilo linaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo pamoja na 
watoto wake wawili waliokutwa wakiishi kwenye nyumba hiyo.
Aidha kamanda Sabas alisema kuwa 
kesho yake polisi waliendelea kufanya upekuzi na kubaini mabox zaidi ya 
20 yenye nyara mbali mbali miongoni mwa nyara hizo alizitaja kuwa ni 
Ngozi za Chui.Simba,Tembo na Mamba pia kulikuwemo vichwa vya 
nyani,chui,swala nyati,pembe za faru ,meno ya tembo na nyingine nyingi 
ikiwemo mfuko wa silaha inayosadikiwa kuhifadhia silaha.
 Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la
 polisi mkoani hapa alisema kuwa Watuhumiwa bado wanashikiliwa na jeshi 
hilo kwa mahojiano na watafikishwa kwenye mahakama pindi upelelezi wa 
tukio hilo utakapo kamilika.
 
 
No comments:
Post a Comment