Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, May 15, 2014

WANAMUZIKI 5 TWANGA HOI KWA DENGUE

MA ya Dengue imezidi kuwa tishio jijini Dar es Salaam, ambapo wanamuziki watano wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’, wamekumbwa na ugonjwa huo, habari zimefika katika dawati la Risasi Mchanganyiko.


Mmoja wa wanamuziki wa Twanga anayesumbuliwa na Homa ya Dengue, Bakari Kasongo ‘Mandela’.

Mtoa habari Hassan Rehani ambaye ni meneja wa bendi hiyo, alizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni na kuwataja wanamuziki hao kuwa ni Badi Bakule, Ramadhan ‘Pentagoni’, Bakari Kasongo ‘Mandela’, Sabrina Mbetembete na Natalia Mbui.

“Nimeshitushwa sana na ugonjwa huu, maana katika maisha yangu ugonjwa ambao nilishawahi kuona unasumbua watu wa sehemu moja kwa wingi kiasi hiki ni Kipindupindu tu, sasa hii dengue ni hatari,” alisema Rehani na kuongeza kuwa wanamuziki hao walikuwa wamelazwa Hospitali ya Mwananyamala na kwamba hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri.

Naye mmoja wa wagonjwa hao, Rama Pentagoni, alipozungumza na mwandishi wetu alisema anaendelea vizuri, huku akiuelezea ugonjwa huo kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu.

No comments: