Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, November 29, 2011

AKI AFUNGA MDOA NA MWANAMKE MREFU


Muigizaji marufu wa filamu barani Afrika AKI amevunja ukapela na kuchua jiko aka mke tayari kuanza safari ya ndoa katika maisha yake.
Aki amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na umbo lake na umahiri wake katika tasnia ya filamu duniani.
Mambo yalikuwa hivi .


BREKING NEWS: JK ATIA SAINI MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA

http://sundayshomari.files.wordpress.com/2011/08/president-jakaya-kikwete_portrait.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.
Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari
ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge
kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao
kilichopita cha Bunge.
Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu
katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.
Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na
mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.
Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye
maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru
kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Novemba, 2011.



KILIMANJARO STARS YAITANDIKA DJIBOUTI MABAO 3:0

HATIMAE KILIMANJARO STARS IMEFANIKIWA KUPATA USHINDI WA KWANZA KWENYE MASHINDANO YA CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP 2011 BAADA YA KUIFUNGA DJIBOUTI MABAO 3-0.
MABAO HAYO YAMEFUNGWA NA THOMAS ULIMWENGU,MWINYI KAZIMOTO NA YUSUF RASHID.
WAKATI HUO HUO RWANDA IMEIFUNGA ZIMBABWE MABAO 2-0 KWENYE MCHEZO ULIANZA MAPEMA.


SOKO LA KISIMANI MJI MDOGO WA TUNDUMA LILIVYOTEKETEA KWA MOTO.


Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya limeteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo. Chanzo hakijaweza kubainishwa lakini inadaiwa kuwa Umeme uliporudi baada ya kukatika ndipo moto ulipoanza katikati ya Soko hilo
Vibanda vilivyokuwa vimejengwa kwa mbao vimeteketea na kubakia masalia ya mabati yaliyotumika kuezekea vibanda hivyo katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya, jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketeakwa moto huo.


Magari ya kampuni ya Ujenzi wa barabara ya Tunduma mpaka Sumbawanga yalifika kutoa msaada wa kudibiti moto katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yaliteketea
Mzee huyu alishikwa na bumbuwazi la kutoamini duka lake likiteketea kwa moto ambapo hivi karibuni aliingiza mzingo wa bidhaa kutoka jijini Dar es salaam uliogharimu shilingi milioni Ishirini

No comments: