



 
  
  
 
Kwa staili hii tutafika mbali katika kiwanda cha mitindo.

MISS TOURISM TANZANIA KWENDA UTURUKI
Mshindi wa tano wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania2010/2011 Sophia Dio na mshindi wa taji la vipaji la Miss Utalii Tanzania
 2010/2011 Dessy Mushumbuzi,wanatarajia kuondoka nchini 19-12-2011 
,kwenda kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss Globe 
International 2011.
Jumla
 ya nchi 120 Duniani zinashiriki katika shindano hilo,litakalofanyika 
30-12-2011 katika jiji la Istanbul na kuonyeshwa Live kupitia TV 
mbalimbali Duniani. Shindano hilo kama lilivyo shindano la Miss Utalii 
Tanzania,linalenga kutangaza na Utalii,Utamaduni wa mataifa mabalimbali 
Duniani,pia kuunganisha na kubadilishana tamaduni miongoni mwa mataifa 
na washiriki.
Hii
 itakuwa ni fulsa nyingine kwa Tanzania kuweza kutangaza utalii na 
utamaduni wetu kimataifa, na hata mianya ya uwekezaji iliyopo Tanzania 
kupitia warembo hawa wa Miss Utalii Tanzania, ambao historia inaonyesha 
kuwa mara zote wanaposhiriki mashindano ya Dunia na kimataifa hutwaa 
mataji mbalimbali. hadi sasa Miss Utalii Tanzania tunashikilia zaidi ya 
mataji 5 ya Dunia,yakiwemo Miss Tourism World 2005- Africa, Miss Tourism
 World 2006 -SADC, Miss Tourism World 2007 - Africa, Model Of The World 
2008 - Personality , Miss Africa 2006 - !ST Runner Up n.k
Tunaendelea
 na maandalizi kuhakikisha tunadumisha na hata kuvuka rekodi ya kwa 
kuahalilisha kuwa warembo hao wanarudi na mataji na sio wasindikizaji 
kama walivyo wengine. Tunaomba makampuni na watu mabalimbali wajitokeze 
kudhamini na kuchangia safari na ushiriki wa warembo hao katika 
mashindano hayo ya Dunia
 
 








No comments:
Post a Comment