Mfalme Mswati wa Swaziland. 
Mabinti
 wa Kiswaziland wakiwa wamevalia mavazi ya kikabila wakati wa sherehe za
 kupita mbele ya Mfalme Mswati ili achague Mke mwingine wa kuoa kama 
mila zao zinavyotaka. 
Askofu Meshack Mabuza. 
Wakati
 vugu vugu linaloendelea katika Mataifa mbali mbali ndani ya Bara la 
Africa, la wananchi kuwatoa watawala ambao wamekaa muda mrefu katika 
madaraka yao, sasa laamia Swaziland kwa Mfalme Mswati. 
Hali
 hiyo imepelekea mpaka viongozi wa dini kuingilia kati kwa kuitaka 
serikali ya Mswati iweze kutoka madarakani na kuitisha uchaguzi ambao 
utakuwa wa kidemokrasia wa vyama vingi. 
Hayo
 yametokea kutokana na utawala wa Mswati kushindwa kuwalipa mishahara 
baadhi ya wafanyakazi wa Serikali kwa wakati husika na kuwaomba wasubiri
 mpaka mwezi wa Disemba na mambo mengine mengi ambayo yanatokea Nchini 
Swaziland. 
Hali
 hiyo pia imetokana na wananchi kuulalamikia utawala wake kuwa ni wa 
kifisadi na kuifanya serikali yake kushindwa kufanya sherehe ya 
kuadhimisha miaka 25 ya utawala wake. 
 
 



No comments:
Post a Comment