 
              
  Kamati
 ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetoa 
onyo la mwisho kwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage na Ofisa Habari 
wa Yanga Louis Sendeu kutokana na kutohudhuria vikao viwili mfululizo 
kama walivyotakiwa na kamati hiyo.
  
 Rage
 na Sendeu wanatakiwa kujieleza mbele ya kamati hiyo iliyo chini ya 
Kamishna mstaafu wa Polisi, (CP), Alfred Tibaigana, kutokana na tuhuma 
za utovu wa nidhamu baada ya kudaiwa kutoa kauli zenye lengo la kushusha
 maendeleo ya soka hapa nchini, wakati wa kuelekea mechi ya Ngao ya 
Hisani, kati ya Simba na Yanga.
  
  Kwa
 mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, kamati hiyo 
inatarajiwa kukaa hivi karibuni ambapo imeagiza Rage ataarifiwe kuwa 
anayepanga vikao vya kamati hiyo sio yeye, hivyo endapo hatatokea siku 
atakayoitwa, atajadiliwa na mamuzi kutolewa.
 AMASHA LA STR8 MUSIC INTER COLLEGE 2011-DODOMANAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA
Naibu Waziri wa 
Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu  (MB) akikata utepe kama ishara
 ya kufungua rasmi maonyesho ya 9 ya SIDO  ya nyanda za juu kusini 
inayoshirikisha mikoa ya Rukwa, Iringa na Mbeya.  Kulia kwake 
anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce  Mgana. 
Maonyesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani  Rukwa
  kwa kushirikisha wajasiriamali kutoka zaidi ya mikoa 14 nchini  na 
wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Burundi.
 
 
No comments:
Post a Comment