Baadhi
 ya washiriki wa shindano la mitindo lililojulikana kama Uni Fashion 
Bash kutoka vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma wakicheza wakati wa 
utambulisho lililofanyika Royal Village Dodoma jana.

  Baadhi
 ya washiriki wa shindano la mitindo lililojulikana kwa Uni Fashion Bash
 kutoka vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma wakicheza wakati wa utambulisho
 wa shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Royal Village mjini 
Dodoma jana.
 

  Mshindi
 wa kwanza wa shindano la wanamitindo lililojulikana kama 'Uni Fashion 
Bash',Respicious Denis (kushoto)kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) 
akipokea zawadi yake ya shilingi laki tano kutoka kwa mwakilishi wa TBL 
kanda ya kati John Tesha, baada ya kutangazwa mshindi katika shindano 
hilo lililofanyika ukumbi wa Royal Village mjini Dodoma jana.

  Baadhi
 ya washiriki wa shindano la ubunifuwa mavazi lililojulikana kwa Uni 
Fashion Bash kutoka vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma wakitambulishwa 
jukwaani wakati wa shindano hilo.

  Mshindi
 wa kwanza wa ubunifu wa mavazi wa shindano la 'UNI fashion Bash' ,Irene
 Rwakatale (kushoto) akipokea akipokea zawadi yake ya shilingi laki saba
 kutoka kwa Meneja wa Redds, Victoria baada ya kutangazwa mshindi wa 
shindano hilo jana.

  Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo malimbali vya mjini Dodoma wakishangilia wakati wa shindano hilo.

  Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo malimbali vya mjini Dodoma wakishangilia wakati wa shindano hilo.

  Mwanamuziki wa kizazi kipya, Mwana FA, akishambilia jukwaa wakati wa shindano hilo.

Mwana FA, akipagawisha na mmoja wa shabiki wake jukwaani wakati wa onyesho hilo.
KAMPUNI
 ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi
 kufutwa kwa mashindano ya 'ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI' 
yaliyotarajiwa kuanza Novemba  22, hadi 26, 2011. 
 Akitangaza
 mabadiliko ya safari hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar 
Shelukindo, alisema kuwa Pamoja na mashindano hayo kufutwa Bia ya 
Safari, imeandaa ziara ya timu ya Taifa ya Pool katika mikoa ifuatayo ya
 Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga baada ya kushauriana na 
chama cha mchezo huo ili kuwafanya wachezaji wa timu ya taifa kuwa 
katika hali ya mchezo na kufanya mazoezi baada ya kuahirishwa kwa 
mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike Malawi.
Aidha 
imeelezwa kuwa kuahirishwa kwa mashindano hayo kufanyika Malawi 
kumefuatia kutokea kwa machafuko ya Kisiasa na hii itatoa nafasi kwa 
mikoa iliyotajwa kuiona timu yao ya Taifa na baadhi ya wachezaji wakali 
wa mikoa hiyo kupata nafasi ya kucheza na wachezaji wa timu yhiyo ya 
Taifa.
RAIS JAKAYA M. KIKWETE ATUA DODOMA RASMI KUHUDHURIA VIKAO VYA CHAMA CHAKE CCM.
Katika Uwanja wa 
ndege wa Dodoma Dkt Kikwete amepokewa na  viongozi pamoja na wana CCM 
wengi wakiongozwa na Makamu wa Rais Dkt  Mohamed Ghalib Bilal na Waziri 
Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni Mwenyekiti  wa Wabunge wa CCM.
Na Mwandishi Maalum, Dodoma, Jumamosi Nov. 19, 2011.
 
 




No comments:
Post a Comment