 Mtu
 mmoja ambaye hajatambulika jina lake amenaswa na umeme wa transfoma 
usiku wa kuamkia leo katika eneo la Hospitali ya Bugando jijini Mwanza 
na kufariki dunia papo hapo.
   Mtu
 mmoja ambaye hajatambulika jina lake amenaswa na umeme wa transfoma 
usiku wa kuamkia leo katika eneo la Hospitali ya Bugando jijini Mwanza 
na kufariki dunia papo hapo.Taarifa za uchunguzi zinamtaja mtu huyo ambaye inasemekana kuwa alikuwa katika mchakato wa kuiba mafuta ya transfoma hilo, wakati akifanya wizi huo alinasa mara baada ya kuegemea bila kujua moja ya nyaya zilizokuwa na umeme.
 Mafundi wa umeme kutoka Tanesco wakipanda kuunasua mwili wa jamaa huyo.
Mafundi wa umeme kutoka Tanesco wakipanda kuunasua mwili wa jamaa huyo. Kutokana
 wizi huo baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza hususani eneo la Hospitali 
ya Bugando na maeneo yake ya jirani yamekosa umeme usiku mzima hadi leo 
na baadhi ya shughuli kusimama kwa kukosa nishati ya umeme.
Kutokana
 wizi huo baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza hususani eneo la Hospitali 
ya Bugando na maeneo yake ya jirani yamekosa umeme usiku mzima hadi leo 
na baadhi ya shughuli kusimama kwa kukosa nishati ya umeme. Asubuhi
 ya leo mashuhuda kutoka sehemu mbalimbali walimiminika kwenye tukio 
hilo la kutisha na kuona hatua kwa hatua za ushushaji wa mwili wa mwizi 
huyo wa mafuta ya transfoma.
Asubuhi
 ya leo mashuhuda kutoka sehemu mbalimbali walimiminika kwenye tukio 
hilo la kutisha na kuona hatua kwa hatua za ushushaji wa mwili wa mwizi 
huyo wa mafuta ya transfoma. TANESCO
 kupitia kitengo chake cha usalama, kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu 
hali hiyo, ili kupambana na wizi huo na licha ya kuwakamata baadhi ya 
wahalifu ambao baadhi yao walifikishwa mahakamani na kesi zao bado 
zinaendelea kusikilizwa kwenye mahakama mbalimbali hapa nchini bado wizi
 unafumuka kwa kasi tena ya ajabu chanzo kikuu kikitajwa kuwa ongezeko 
la mahitaji.
TANESCO

la mahitaji. Kila
 kukicha TANESCO imekuwa ikingia gharama katika kununulia vifaa 
vilivyoibwa badala ya kuendeleza maendeleo ya miradi ya umeme nchini.
Kila

No comments:
Post a Comment