WAZIRI MWANDOSYA AREJEA NYUMBANI
Waziri
 wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya
 Apollo, nchini India, kwa takriban miezi minane, amerejea nchini, baada
 ya afya yake kuimarika. Habari
 zilizopatikana jijini Dar es Salaam zilizothibitishwa na Naibu Waziri 
wa Wizara hiyo, Mhandisi Gerson Lwenge, Profesa Mwandosya alirejea 
nchini juzi. Mwingine
 aliyethibitisha jana kurejea kwa waziri huyo mwandamizi, ni mkewe, Lucy
 Mwandosya. Hata hivyo, Mhandisi Lwenge, ambaye alizungumza na 
jana, alipotakiwa kueleza maendeleo ya afya ya Waziri Mwandosya, 
alijibu: “Sijamuona, ndio naenda. Ukinitafuta baadaye nitakwambia.” Awali,
 Mhandisi Lwenge, alipoulizwa kama Waziri Mwandosya amerejea nchini, 
alijibu: “Ndio amerudi” na alipotakiwa kueleza lini alirejea, alijibu: 
“Jana (juzi).” Baadaye,
 majira ya saa 11.05 jioni jana, ilimtafuta Profesa Mwandosya 
kwa simu yake ya mkononi, ambayo ilipokelewa na mkewe, Lucy. Baada
 ya mwandishi kujitambulisha na kueleza shida yake ya kutaka kuzungumza 
na Profesa Mwandosya, Lucy, alisema muda huo waziri asingeweza 
kuzungumza kwa vile alikuwa anapumzika.
MILIONI 55 ZAKUSANYWA RED RIBBON FASHION SHOW
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
MILIONI 55 ZAKUSANYWA RED RIBBON FASHION SHOW
WAKATI jumla ya  sh.
  Milioni 55 zimechangishwa katika maonyesho ya mitindo kwa ajili ya  
kuadhimisha siku ya ugonjwa hatari wa UKIMWI duniani (Red Ribbon Fashion
  Gala),  mwanamuziki nyota nchini, Diamond aling’ara vilivyo kwa kuonyesha kipaji kingine cha maonyesho ya mavazi.
Fedha
  hizo zilipatikana kwa njia ya mnada wa vitu mbali mbali na nyingine  
zikitolewa kwa njia ya udhamini wa shughuli hiyo iliyotumika pia  
kuadhimisha siku ya ugonjwa hatari wa Ukimwi Duniani.
Mkurugenzi
  Mtendaji wa Tanzania Mitindo House (TMH), Khadija Mwanamboka  
aliwashukuru wadau wa maonyesho ya mavazi kwa kujitolea kufanikisha  
kupatikana kwa fedha hizo ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo
  cha mafunzo ya fani mbali mbali kwa watoto yatima wanaoishi na virusi 
 vya Ukimwi.
Mwanamboka
  alisema kuwa kituo hicho kitajengwa jijini na kitatoa mafunzo ya njia 
 mbali mbali za kupambana na maisha, Ujasiliamali, Ushonaji nguo, 
mafunzo  ya kompyuta na jinsi ya ubinifu wa mitindo au mavazi. Alisema 
kuwa  jumla ya watoto yatima 100 watakuwa wanapata mafunzo katika kituo 
hicho  kila mwaka.
Baadhi
  ya wadhamini waliochangia kufanikisha kwa fedha hizo ni kampuni ya 
simu  ya mkononi, Vodacom Tanzania na wadau wa maonyesho ya mavazi ambao
  walichangia kimya kimya katika maonyesho hayo yaliyofanyika kwenye 
hotel  ya Double Tree.
Katika
  maonyesho hayo, mkali wa miondoko ya Bongo Fleva nchini, Diamond naye 
 alifanya vitu vyake jukwaani kwa kuvaa nguo aina ya Kidoti iliyobuniwa 
 na mbunifu chipukizi, Jokate Mwegelo.
Wengine
  walioonyesha mavazi jukwani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark  
Production, Ritha Poulsen ambaye baadaye nguo yake iliunuliwa na mcheza 
 filamu maarufu nchini, Steven Kanumba.
Wabunifu
  mbali mbali akiwemo Doreen Estazia nao walionyesha mavazi yao, Doreeen
  alionyesha mitindo yake maarufu ya Eskado Bird. Wabunufu wengine  
waliotamba katika maonyesho hayo ni Ali Rhemtullah, Diana Magese, Mollel
  na Zamda. 
Wadhamini
  wengine wa shughuli iyo walikuwa Redds, Clouds Entertainment, Kiondo  
Communications, I_View Media team na Hall Neel Production. Wengine  
waliosaidia maonyesho hayo ya mavazi ni Amaya Beauty Saloon and SPA,  
Bank M Tanzaniia, Stanbic Bank, Mimis collections, Kidoti By Jokate  
Mwegelo, Bongo Real Mamaz na Bluecherriemoe.
Wadau wengine ni Flaviana Matata Foundation,  Amina
  Design, Jenifa Pemba, FM Express events and services ltd, Ernst  
&Young, ,LR Creations, Millen Magese Foundation Tiffex, Cool Blue  
Iku Lazaro, Miraj Kikwete, Halima Kamus, Mabibo Beer Wines nd Spirits  
Ltd, and World Link Travel and Tours ltd.
 
 

No comments:
Post a Comment