Mtangazaji  wa Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC – HALIMA MCHUKA amefariki dunia  usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI Jijini DSM  alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa kiharusi.
Kwa  mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC CLEMENT MSHANA, HALIMA MCHUKA  alikimbizwa katika hospitali ya DAR GROUP na baadae katika hospitali ya  Taifa ya MUHIMBILI hapo jana baada ya kuanguka ghafla akiwa katika kituo  chake cha kazi eneo la PUGU ROAD Jijini DSM.
MCHUKA alikuwa mtangazajii wa kwanza wa kike wa mpira AFRIKA MASHARIKI.
 
 

No comments:
Post a Comment