Eneo  hili linaitwa Wawili Wapendanao na hapa ni Karatu Barabara yanapopita  mabasi yaendayo Mwanza, ni maarufu kutokana na huu mti unaoonekana  pichani ambao umeshindikana kwa namna yeyote kuuondoa ama kuukata mahala  hapa. 
Wenyeji  wa maeneo haya wameuambia Mtandao wa Sufianimafoto kuwa, hata wajenzi  wa Barabara hii walijaribu kutaka kuukata bila mafanikio kwani haukatiki  wala haung'oki pamoja na kwamba walijaribu kila njia ikiwa ni pamoja na  kufuata mila za kiswahili zilizoelekeza kuukata mti huo usiku wa manane  bila mafanikio. 
Aidha  imeelezwa kuwa mti huo pia umekuwa maarufu zaidi kutokana na kutokea  ajali za mara kwa mara katika mti huo na kuua watu, ambapo  tayari zimekwishatokea ajali kadhaa ikiwa ni pamoja na ajali mbili za  wanandoa waliotoka kufunga pingu za maisha na wakati wakirejea kuelekea  ukumbili safari yao ikaishia katika mti huu na hiyo ilikuwa ni mwaka  jana tu, wakati mwaka juzi pia ilitokea ajali kama hiyo ya kusikitisha  mahala hapa. 
 
 

No comments:
Post a Comment