 MWANAMUZIKI  mahiri wa miondoko ya dansi aliyepata kujizolea sika kem kem nchini  wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda  kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica, Ndanda Cosovo  ‘Kichaa’ amekamatwa masaa machache jijini Arusha pamoja na wanamuziki wa  bendi yake mpya.
MWANAMUZIKI  mahiri wa miondoko ya dansi aliyepata kujizolea sika kem kem nchini  wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda  kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica, Ndanda Cosovo  ‘Kichaa’ amekamatwa masaa machache jijini Arusha pamoja na wanamuziki wa  bendi yake mpya.
Akizungumza  na Mtandao wa Sufianimafoto kwa njia ya simu, Ndanda Cosovo, alisema  kuwa amekamatwa yeye pamoja na wanamuziki wake wote na kuwekwa chini ya  ulinzi ambapo kwa sasa wanasubiri kupelekwa Rumande hadi kesho  watakaposafirishwa kurudi kwao Kongo.
 Aidha  Ndada alisema kuwa ameshangazwa na uongozi wa Uhamiaji kukagua vibali  vyake vya kuishi nchini na kumwambia kuwa vibali hivyo ni ‘Feki’ hali ya  kuwa alikata na kulipia vibali hivyo jijini Dar es Salaam.

“Mimi  nashangaa sana kama Mkurugenzi wa Uhamiaji anaweza kupokea pesa na  kisha akatoa vibari Feki, hii si sawa kwani mimi nilikuwa nikiishi  Tanzania kwa uhalali na kufuata taratibu zote na ndiyo maana nikawa  nikifanya kazi zangu bila kificho, leo nakamatwa nakuambiwa vibari  vyangu ni feki kwa kweli nimesikitika sana, 
 Napenda  kuwaageni marafiki zangu wote mbaki salama kwani tuliishi kwa amani na  kusaidiana kama ndugu leo hii naambiwa nimevunja sheria mbona  hawajaniambia hivyo tangu nilipokuwa nikiwalipa pesa za vibari??”  alimaliza kwa kuhoji Cosovo. 
KILIMANJARO STARS YATINGA NUSU FAINALI CECAFA CUP
 
                  Timu  ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars imefanikiwa kuingia nusu  fainali ya CECAFA Senior Challenge Cup 2011, baada ya kuifunga timu ya  Malawi kwa goli moja kwa bila. Goli la Stars lilifungwa na kiungo Nurdin  Bakary katika kipindi cha kwanza na kudumu mpaka mwisho wa mchezo.
  Kwa matokeo hayo Kili stars sasa itacheza na Uganda katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali siku ya Alhamisi. 
 
 
No comments:
Post a Comment