 
              
David Beckham amekiri alikataa ofa nyingi kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuamua kusaini mkataba mpya na Los Angeles Galaxy
  
Mkataba
 wa miaka mitano wa Beckham na Galaxy uliisha mwezi uliopita na alikuwa 
anauhusishwa kwa kiasi kikubwa kujiunga na Paris Saint Germain.
  
Ingawa, ameamua kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na LA galaxy, timu ambayo alishinda nayo taji la MLS in 2011.
  
“Huu
 ulikuwa uamuzi muhimu zaidi kwangu. Nilikuwa na ofa nyingi sana kutoka 
sehemu tofauti duniani, lakini kutokana na sababu tofauti ikiwemo 
mapenzi yangu ya kuendelea kucheza America na kushinda makombe na 
Galaxy.
  
“Nimeshuhudia
 sasa ni jinsi gani soka lilivyo maarufu hapa States na nimeamua 
kuendelea kushirikiana na wadau wengine kuuukuza huu mchezo hapa.
  “Familia
 yangu na mimi mwenyewe tuna furaha sana hapa, na sasa tunaangalia mbele
 kuendelea kuishi hapa kwa amani na furaha zaidi.” Alimaliza Beckham.
 
 
No comments:
Post a Comment