Kutoka eneo
 la tukio mmoja Kati ya abiria walionusurika katika ajali hiyo John 
Sanga alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha basi kwa 
mwendo kasi na uzembe mwingina hata abiria walipojaribu kumkanya 
alishindwa kusikiliza. Katika
 ajali hiyo abiria wengine zaidi ya 16 walijeruhiwa vibaya na kulazwa 
katika hospital ya wilaya ya Mufindi huku wengine zaidi ya 20 wakipata 
michubukomidogo midogo na kutibiwa na kuruhusiwa .Mashuhuda wa ajali 
hiyo walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa ajali hiyo ilitokea 
majira ya saa 9 alasiri Leo wakati basi hilo likielekea mkoani Mbeya na 
kuwa chanzo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva. Alisema
 eneo hilo ambalo ajali imetokea ni eneo ambalo linamteremko na kuwa 
mbali ya basi hilo kupinduka pia magari mengine Mawili likiwemo gari la 
serikali lenye namba za usajili STK 2340 na IT yamegongana na Lori 
katika eneo hilo. Maiti zilizotolewa katika ajali hiyo hadi saa 2.usiku 
zilikuwa ni nne na hadi mwandishi wa habari hii anatoka eneo la tukio 
jitihada za kunyanyua basi hilo ilikutazama maiti nyingine lilikuwa 
likieendelea chini ya usimamazi wa mkuu wawilaya ya Mufindi Evarista 
Kalalu na mkuu askari wa Kikosi cha usalama barabarani wakiongozwa na 
mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Kedmundi Mnubi 
lilikuwa likiendelea . Majeruhi
 wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika hospital hiyo ya wilaya ya Mufindi
 ni pamoja na mtoto wa kiume wa mwaka mmoja ambaye mama yake alikufa 
katika ajali hiyo , Alen Kilima mkazi wa Kyela , Mwanahabari wa radio 
Kyela Fm Prakseda Mburu (24) ,Maria Mtawa (46) mkazi wa Tukuyu,Lutusyo 
Kabenjela (45) mkazi wa Kyela, Elizabeth Andwer(27)Dina Mwasongela (14) 
mwanafunzi wakidato cha tatu sekondari ya Lutengano Mbeya,Alex Mwaibambe
 (28) mwanafunziwa mwaka wa pili injinia katika chuo kikuu cha Dar es 
Salaaam ,Amon Luvanga(30) mkazi wa Mbeya,Yohana Mwasomola(28) Wengine
 ni Aggrey Mwangulu (56) mfanyakazi wa TRA Kibaha , Runna Mwampate (36) 
mkazi wa Kilawani Dar es Salaam , Iman Mwakifwage (32) mkazi wa Mbeya 
Mbali
 ya majeruhi hao kulazwa katika Hospital ya wilaya ya Mufindi baadhi ya 
majeruhi walikimbizwa katika Hospital ya wilaya ya Ilembula wilayani 
Njombe. Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Claus Mwasyeba 
alithibitisha kutokeakwa ajali hiyo na kuwa majeruhi Ramadhan Kipangule 
(28) mkazi wa TukuyuMbeya amefariki usiku wa leo wakati akipatiwa 
matibabu katika Hospital ya wilaya ya Mufindi. Alisema kuwa kati ya 
abiria waliokufa katika ajali hiyo watatu ni wanawake na abiria wawili 
ni wanaume na mmoja ametambuliwa kwa jina la ramadhan Kipangule (28) 
mkazi wa Uyole Mbeya . Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi 
linaendelea kumsaka dereva wa basi hilo Yahaya Abdalla (35) mkazi wa Dar
 es Salaam na msaidizi wake Nasib Salum ambao baada ya ajali hiyo 
walikimbia.Mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista kalalu amewataka wananchi 
popote pale nchini kujitokeza kutambua miili ya marehemu hao akiwemo 
mwanamke huyo aliyeacha mtoto wa mwaka mmoja na nusu.
 
 
No comments:
Post a Comment