Jeshi
 la Nigeria linasema limewapiga risasi na kuwauwa wafuasi 11 wa kikundi 
cha wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, kaskazini-mashariki mwa nchi. Msemaji
 wa jeshi alieleza kwamba wapiganaji hao waliuwawa wakati wa mapambano 
katika mji wa Maiduguri, ambako kundi hilo lilianzishwa mwongo 
uliopita. Juma lilopita watu kama 185 waliuwawa katika mji mwengine wa kaskazini, Kano, kwenye mashambulio kadha ya mabomu. Boko Haram ilisema ilifanya mashambulio hayo, na imeonya kuwa itaendelea na ugaidi hadi mfumo wa sharia unafuatwa Nigeria nzima.
 
 
No comments:
Post a Comment