
Mahakama
 ya  hakimu mkazi Kisutu,  leo imeshindwa kumsomea maelezo ya awali, 
yaani PH,   aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania 
(ATCL), David Mattaka na  wenzake wawili kutokana na  mawakili wa upande
 wa utetezi kushindwa kufika  mahakamani hapo.
 
Mataka
  anakabiliwa na makosa matatu likiwemo kosa la matumizi mabaya ya 
madaraka  kinyume na Sheria na kifungu 31 Na.11 ya Kuzuia na Kupamba na 
Rushwa Na.11 ya  mwaka 2007.
 
Washtakiwa
   wengine  katika kesi hiyo  ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha 
Elisaph  Mathew Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William  
Haji.
 
Katika
  shtaka la kwanza linalowahusu washtakiwa wote  kwa pamoja wanadaiwa 
kuwa  walishindwa kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya manunuzi 
waliyokuwa wakifanya  na mtoa huduma kinyume na kifungu cha 55 (3), 87 
(1) (f) cha Sheria ya Manunuzi  ya Umma Na. 21 ya mwaka 2004 na kanuni 
ya 17(1) ya Sheria ya Manunuzi (Goods,  Works, Non-Consultant Services 
and Disposal of Public Asets by Tender)  Regulation, G.N. No.97 of 2005.
 
Upande
 wa  mashtaka unadai  shtaka la pili ambalo pia linawakabili washtakiwa 
wote ni la  kushindwa kutimiza matakwa ya vifungu vya Sheria ya Manunuzi
 ya Umma na Kanuni  zake kinyume na kifungu cha 87 (1) (f) cha Sheria ya
 Manunuzi ya umma ya mwaka  2004.
 
Shtaka
 la  tatu linalo mkabili Mattaka pekee  linahusu  matumuzi mabaya ya 
madaraka kinyume  na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na 
Rushwa ya mwaka  2007
 
Mara
 tu  baada ya kesi hiyo kuanza, mapema leo asubuhi upande wa mashtaka 
ukiongozwa na  mwendesha mashtaka kutoka TAKUKURU, BENY LINCOLYNE, 
ulieleza kuwa uko tayari kwa  ajili ya  kesi hiyo ambapo hata hivyo 
hakimu , RITTA TARIMO alilazimika  kuiahirisha mpaka Februari 23 mwaka 
huu baada ya kuona kwamba  mawakili wa  utetezi hawakuwemo katika chumba
 cha mahakama ilikokuwa ikiendeshwa kesi  hiyo.
 
 
No comments:
Post a Comment