 
  
Nahodha
 wa timu ya Taifa ya mpira  wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), Sophia 
Mwasikili ameondoka jana alfajiri  (Januari 30 mwaka huu) kwa ndege ya 
Turkish Airlines kwenda Uturuki kucheza  mpira wa kulipwa. 
Mwasikili amekwenda kujiunga na  Luleburgazgucu Spor Kulubu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake nchini  humo. 
Beki
 huyo wa kati wa Twiga Stars  aliyekuwa akichezea timu ya Sayari Women 
amejiunga na klabu yake hiyo mpya kwa  mkataba wa miaka miwili. 
Awali
 Mwasikili alitakiwa kujiunga  mapema na timu hiyo lakini alilazimika 
kusubiri kwanza mechi ya marudiano ya  Kombe la Afrika kwa Wanawake 
(AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia (Brave  Gladiators) iliyochezwa 
Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
 
 
No comments:
Post a Comment