Wanafunzi
   wa Shule ya Msingi Nsenga jijini Mbeya wakitoka kushuhudia mwili wa  
 mwanafunzi mwenzao wa darasa la Kwanza Silvia Isaya (5) alieuawa kisha 
  viungo vya mwili wake kunyofolewa ulimi, jicho la upande wa kushoto,  
 sehemu za siri na mguu wake wa kushoto kuvunjwa.
 Baadhi
   ya wananchi wa Nsenga jijini Mbeya wakishuhudia mwili wa mwanafunzi 
wa   darasa la Kwanza Silvia Isaya (5)  alieuawa kisha viungo vya mwili 
 wake  kunyofolewa ulimi, jicho la upande  wa kushoto, sehemu za siri na
  mguu  wake wa kushoto kuvunjwa.
 Mwili
   wa marehemu ilvia Isaya (5)  alieuawa kisha viungo vya mwili wake   
kunyofolewa ulimi, jicho la upande  wa kushoto, sehemu za siri na mguu  
 wake wa kushoto kuvunjwa ukiwa umefunikwa kwa kitenge, kutokana na   
kuharibika vibaya hivyo kushindwa kuuonesha.
Mwenyekiti
   wa Kijiji cha Nsenga Bwana Gibson Mwaselela (mwenye koti la rangi ya 
  Samawati ), Baadhi ya wananchi wa Nsenga jijini Mbeya wakishuhudia 
mwili   wa mwanafunzi wa darasa la Kwanza Silvia Isaya (5)  alieuawa 
kisha   viungo vya mwili wake kunyofolewa ulimi, jicho la upande  wa 
kushoto,   sehemu za siri na mguu wake wa kushoto kuvunjwa AKIRIPOTI 
Ezekiel   Kamanga.
Hitimisho:-
   Wimbi la mauaji dhi ya watoto limezidi kutanda mkoani  Mbeya baada ya
   watoto wawili kuawa katika nyakati tofauti  na watu wasiojulikana na 
  kisha kunyofolewa sehemu za siri, ulimi na jicho la kushoto Wilaya ya Rungwe na Mbeya.
Kufuatia
   tukio hilo jumla ya wananchi 14 walikamatwa na Jeshi la polisi lakini
   machifu waliingilia kati, ambapo mtu mmoja aitwaye Joseph Mwangolobe 
 (40  - 45) , mkazi wa Kiwira alijitokeza na kukiri kuwa ndiye  
aliyehusika na  mauaji hayo chumbani kwake.
Jeshi
   la polisi lilifanya kazi ya ziada kumnusuru Joseph asiuawe na 
wananchi   wenye hasira kali baada ya wananchi hao kutaka kulipiza 
kisasi, na   familia yake imelazimika kuhama ikiwa chini ya ulinzi wa 
polisi.
Baba
   mzazi wa mtoto Silvia Isaya (5) Bwana Isaya Samson Mwalyego amesema  
 alimwacha mwanawe Silvia majira ya saa 11:00 jioni Januari 13, mwaka 
huu   alipokuwa anakwenda kazini Hoteli ya Silver Coin, hali mama yake  
 akienda kutafuta mahitaji ya nyumbani kwa ajili ya mlo wa usiku.
Mama
   mzazi alipomaliza kupika alimtafuta mwanae pasipo mafanikio hivyo   
alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji cha Nsenga Bwana Meshack Mwaipasi 
  ambapo walitafuta usiku huo  bila mafanikio.
Asubuhi
   majira ya saa 2 kamili  Januari 24, mwaka huu mwili wa mtoto huyo   
ulipatikana katika shamba la mahindi Kitongoji cha Isenyela Kata ya   
Nsenga ukiwa umeondolewa baadhi ya viungo na mwili wa mtoto huyo   
ulichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa kwa uchunguzi zaidi.
   
Kamanda
   wa Polisi Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na   
kwamba uchunguzi unafanyika ilikuweza kuwabaini waliohusika na tukio   
hilo la kikatili.
 
 
No comments:
Post a Comment