Makamu
 wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal 
ametuma salamu za  rambirambi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini 
Inspekta Jenerari Said  Mwema na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa, 
kufuatia ajali ya gari  la Polisi lililopata ajali na kusababisha kifo 
cha askari sambamba na  kujeruhi wengine, ajali iliyotokea jana katika 
barabara itokayo Lushoto  kuingia mji mdogo wa Mombo, gari ambalo 
lilikuwa mwishoni mwa msafara  wa Makamu wa Rais uliokuwa ukitokea 
wilayani Lushoto. 
Makamu
 wa Rais alikuwa  akimalizia ziara yake mkoani Tanga, ziara aliyoianza 
Januari 24 na kuikamilisha jana Januari 27 wilayani Lushoto. Msafara wa 
Makamu wa Rais ulikuwa unatoka  Lushoto ukielekea Hale, ambako huko 
Makamu wa Rais amefika salama. Makamu  wa Rais amesikitishwa sana na 
tukio hilo na amewapa pole Mkuu wa Jeshi  sambamba na Mkuu wa Mkoa wa 
Tanga, na anabainisha kuwa tukio hilo limemgusa  sana na anawatakia moyo
 wa ujasiri na uvumilivu kufuatia tukio hili  ambalo limekuja katika 
kipindi ambacho hakikutarajiwa. 
Makamu
 wa Rais anatarajiwa  kuondoka mjini Tanga kesho kufuatia kuhitajika 
kusimamia mkutano wa  Kamati ya Muungano unaofanyika kesho asubuhi 
jijini Dar es Salaam, sambamba  na kusimamia majukumu mengine ya 
serikali kufuatia Mheshimiwa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
Dkt. Jakaya Kikwete kuwa nje ya nchi  kikazi kwa sasa.“Naamini mkoa wa 
Tanga na Jeshi la Polisi watatoa  huduma zote zinazohitajika kwa wafiwa 
sambamba na majeruhi, nami binafsi  nitafatilia kwa ukaribu,” anasema 
Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal.
 
 
No comments:
Post a Comment