Mtoto
 mdogo wa kike anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka tisa,amelazwa wadi 
namba saba katika Hosiptal ya Mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi akiuguza 
majeraha aliyoyapata yanayodaiwa kutokana na kipigo ambacho amekuwa 
akikipata kutoka kwa shangazi yake ambaye ni Mwalimu wa shule ya Msingi 
Narumu iliyopo wilaya ya Hai.  Mtoto
 huyo ambaye kwa sasa ameathirika kisaikolojia kutokana na tukio 
hilo,inadaiwa na wasamalia wema kuwa,mwanamke huyo amekuwa akimpa vipigo
 mara kwa mara kwa kutumia waya.  Taarifa
 ya jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro iliyotolewa kwa vyombo bya habari
 imedhibitisha ukatili dhidi ya mtoto huyo na kwamba mtuhumiwa 
aliyetajwa kwa jina la Anna John(28)mkazi wa mtaa wa  Kiusa katika 
Manispaa ya Moshi, bado anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.  Kukamatwa
 kwa mtuhumiwa huyo ni matokeo ya wanawake wanaojihusisha na uuzaji wa 
mboga mboga na matunda  wa mtaa wa Kiusa mjini Moshi kuamua kufuatilia 
nyendo za mtoto huyo baada ya kutumwa sokoni na mtuhumiwa na kisha 
kurejea tena sokoni akiwa analia na kuwapa hofu kina mama waliokuwa 
sokoni na kuhoji kulikoni. 
 
 
No comments:
Post a Comment